Pambazuko FM Radio

Ufugaji wa kisasa wavuna mamilioni Morogoro

23 June 2026, 19:54

Picha ya Afisa Mifugo Kata ya Katindiuka (haihusiani moja kwa moja na tukio la habari hii) (Picha kwa hisani ya Steven Afisa Mifugo Katindiuka)

Inaelezwa kuwa udhibiti wa magonjwa ni njia muhimu ya kuongeza tija na kupunguza hasara kwa wafugaji

Na Henry Bernad Mwakifuna

Dokta Khamis Nyoni, Mkufunzi kutoka Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Morogoro, amesema kuwa ufugaji bora unaweza kumwezesha mfugaji kupata faida kubwa.

Ameeleza kuwa mbuzi anaweza kuuzwa kwa hadi shilingi milioni 9, na wiki hii ng’ombe mmoja ameuzwa kwa shilingi milioni 15 katika eneo la Ubena Zomozi, Mkiani Morogoro.

Akifafanua zaidi, Dokta Nyoni amesema kuwa matumizi ya vinasaba husaidia kuzalisha mifugo yenye misuli mingi na uzito mkubwa, huku ng’ombe wa maziwa wakitoa maziwa kwa wingi.

Aidha, amesisitiza kuwa udhibiti wa magonjwa ni nguzo muhimu ya kuongeza tija na kupunguza hasara kwa wafugaji.

Picha ya Dokta Khamis Nyoni, Mkufunzi kutoka Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Morogoro,Picha na Henry Bernad Mwakifuna)