Pambazuko FM Radio

Wanafunzi walalamikia vikwazo vya Tahasusi

16 June 2026, 14:48

Baadhi ya wanafunzi katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara wamesema walimu, wazazi na walezi huathiri uchaguzi wao wa tahasusi na masomo, na hivyo wito kutolewa kwa wadau wa elimu kuunda mazingira yatakayowasaidia wanafunzi kufikia ndoto zao za kitaaluma.

Na: Henry Mwakifuna

Baadhi ya wanafunzi katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, wamesema  baadhi ya walimu, wazazi ama walezi na ndugu wamekuwa miongoni mwa vikwazo vinavyowakwamisha kufanya uchaguzi sahihi wa tahasusi na masomo wanayoyapenda.

Wanafunzi hao wameeleza kuwa baadhi ya walimu huwakatisha tamaa kwa kuwaambia kuwa hawana uwezo wa kufanya masomo ya sayansi, hali inayowafanya baadhi yao kushindwa kuendelea na masomo hayo. Aidha, wamesema mbinu za ufundishaji zisizovutia zimechangia wanafunzi wengi kutopenda baadhi ya masomo.

Sauti za wanafunzi

Akizungumza katika kipindi cha Tuzungumze Elimu cha Pambazuko FM, mwalimu wa Shule ya Sekondari Kilamsa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, Bw. Mbembela, amesema mbinu dhaifu za ufundishaji zinaweza kuchangia mwanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika masomo yake. Amesisitiza kuwa mwalimu ana wajibu wa kumshawishi mwanafunzi kulipenda somo analofundisha na kumjengea ari ya kujifunza.

Mwl Mbembela shule ya sekondari Kilamsa

Ameongeza kuwa ndugu, majirani na watu wa karibu mara nyingi huchangia changamoto za ufaulu kwa wanafunzi kupitia mitazamo hasi kuhusu baadhi ya masomo, hususan masomo ya sayansi. Hivyo, ametoa wito kwa wadau wote wa elimu kushirikiana kujenga mazingira rafiki yatakayowawezesha wanafunzi kufanya uchaguzi sahihi wa tahasusi kulingana na uwezo, vipaji na ndoto zao za baadaye.

Sauti ya mwl mbembela