Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
17 August 2026, 15:18

”Majengo yote ya Serikali katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara yafanyiwe tathmini na Tanesco ili kupata huduma ya Umeme akitolea mfano shule ya Sekondari ya Ihanga ambayo imejengwa lakini haina Umeme”-Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Kassim Nakapala.
Na Henry Mwakifuna
Halmashauri ya Mji Ifakara imewaomba shirika la umeme nchini TANESCO Kufanya tathimini ya majengo ya Serikali yasiyo na umeme kwa ajili ya kufanya maamuzi ya pamoja na kupeleka Huduma katika majengo hayo.
Akitoa jibu ya Nyongeza la Kaimu Mkurugenzi wa Mji Ifakara kwenye Baraza la Madiwani la Robo ya Nne ,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Kassimu Nakapala amesema kuwa kutokana na uhitaji wa Nishati kwa Baadhi ya Majengo ya Shule za Msingi na Sekondari za Halmashauri hiyo ni Vyema Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara ikawasilisha ombi la kufanyiwa Tathimini kwa majengo yote ya Serikali.

Msingi wa Jibu hilo ulitokana na Swali lililoulizwa na Diwani wa Kata ya Lumemo Mji Ifakara Frank Ngao, ni lini serikali itapeleka umeme katika sekondari ya Ihanga iliyojengwa kwa zaidi ya milioni 528 kwa ajili ya uboreshaji wa kujifunza na ujifunzaji/ huku akiongeza kuwa wamepokea vifaa vya naabara tayari
Awali kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ifakara Mji, Rashidi Semgoya aliliambia baraza la madiwani kuwa mpaka sasa Halmashauri kwa kushirikiana na Tanesco katika mpango wao wapo katika Tathimini.

Picha ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Rashidi Semgoya