Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
6 November 2026, 14:33

Baadhi ya Wanananchi wa Kiyonjo waliojitokeza katika uchimbaji wa Mitaro Picha na Nicolatha Mpaka
tunaiomba Serikali kutuunga mkono katika jitihada hizi ili kupunguza hatari ya mafuriko na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa mvua–Wananchi
Na Nicolatha Mpaka
Wakazi wa Mtaa wa Kionjo, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, wamejitokeza kuchimba mitaro ya kupitisha maji ili kujikinga na mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua za El Niño na masika.
Wakizungumza na Redio Pambazuko FM, wananchi wamesema changamoto wanazokabiliana nazo wakati wa mvua zimewafanya kuanza maandalizi mapema kwa kuchimba mitaro ya kupitisha maji.

sauti za wananchi
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kionjo, Zuberi Kambangwa, maarufu Muhumini, amesema wananchi wamekubaliana kujitolea kuchimba mitaro hiyo kwa utaratibu maalumu ili kuhakikisha zoezi linafanikiwa.
Hata hivyo, ameiomba Serikali kuongeza nguvu katika jitihada hizo kwa kuwapatia msaada utakaowawezesha kukabiliana na changamoto za mvua.