Pambazuko FM Radio

Kuwalinda nyani ni kuchangia uhifadhi wa Asili

22 October 2026, 11:00

Ni miongoni mwa Vinara wa Mnyororo wa Uhifadhi kwa usambazaji wa mbegu na mfumo mzima wa Ikolojia-Mtafiti

Na Henry Mwakifuna

Jamii imetakiwa kutambua umuhimu wa nyani katika uhifadhi wa mazingira na kuepuka kuwadhuru, kutokana na mchango wao katika usambazaji wa mbegu, uendelevu wa misitu na kudumisha uwiano wa viumbe hai katika mazingira ya porini.

Akizungumzia umuhimu wa nyani, Samwel Mtoka  Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), ameeleza kuwa wanyama hao wana nafasi muhimu katika mfumo wa ikolojia, ikiwemo kusaidia mimea kuenea na kukua katika maeneo mbalimbali.

Amesema nyani wanapokula matunda, mbegu hupitia katika mfumo wao wa mmeng’enyo wa chakula na kutawanywa kupitia kinyesi katika maeneo tofauti. Utaratibu huo husaidia mbegu kufika sehemu mpya, kuota na kukua, hivyo kuchangia uendelezaji wa uoto wa asili na urejeshaji wa misitu.

sauti ya Mtafiti

Kwa ujumla, uhifadhi wa nyani ni sehemu ya juhudi pana za kulinda mazingira, bioanuwai na uendelevu wa mifumo ya ikolojia. Kuwalinda nyani ni kuchangia uhifadhi wa asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.