Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
20 October 2026, 14:26

Baadhi ya Watumishi na Wafanyabiashara wakiwa katika Kikao na Kamishana Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Tanzania picha na mpiga Picha
kuanzia Jumatatu Wataalamu wa Mkoa na wa Makao makuu watakuwa hapa kuanza kutatua ukaguzi wa Makadirio ya Kodi-Kamishna Mkuu TRA.
Na Henry Mwakifuna
Changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wilayani Kilombero zinatarajiwa kuanza kushughulikiwa kuanzia Jumatatu, Oktoba 26, 2026, baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuahidi kupeleka timu ya wataalamu mjini Ifakara.

Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Tanzania TRA Yusufu Mwenda akizungumza na Wawakilishi wa Wafanyabiashara Mjini Ifakara picha na Mwandishi
Kamishna Mkuu wa TRA, Yusufu Mwenda, amewaeleza wawakilishi wa wafanyabiashara hao kuwa timu ya wakaguzi na wataalamu kutoka mkoani na Makao Makuu ya mamlaka hiyo itafika Ifakara kuanza kushughulikia changamoto zilizowasilishwa.
sauti ya Kamishna Mkuu TRA
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara, Katibu wa wafanyabiashara hao amesema ukosefu wa elimu kuhusu taratibu za ununuzi na uuzaji pamoja na utunzaji wa kumbukumbu za biashara ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara.
Sauti ya Katibu wa wafanyabiashara
Kwa upande wake, Didas Kessy wa Kessy Hardware ameiomba TRA kuangalia changamoto za ukaguzi wa kodi, akieleza kuwa kufuata taratibu za ukaguzi katika ofisi za TRA mkoani Morogoro ni changamoto kwa wafanyabiashara wa Kilombero.
sauti ya Mfanyabiashara Kessy