Pambazuko FM Radio

DC Kyobya Azitaka NGOs Kilombero Kuimarisha Ushirikiano na Ubunifu

5 October 2026, 16:30

Muwe wabunifu katika kutatua changamoto za wananchi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa mazingira, akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali na mashirika hayo ni muhimu–Wakili Dunstan Kyobya

Wakili Dunstan Kyobya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akizungumza na Viongozi wa Taasisi Zisizo za Kiserikali NGO katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya Mjini Ifakara Picha na Kuruthum Mkata

Na Kuruthum Mkata

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, amezitaka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wilayani humo kuimarisha umoja, ushirikiano na ubunifu ili kuongeza mchango wao katika kuboresha maisha ya wananchi.

Akifungua Jukwaa la Mwaka la Mashirika ya Kiraia Oktoba 2, 2026 katika Ukumbi wa DC uliopo Kata ya Kibaoni, Ifakara, Kyobya amesema ushirikiano utaziwezesha NGOs kubadilishana uzoefu, kufahamiana zaidi na kuibua fursa za maendeleo kwa taasisi zao.

Aidha, amezitaka NGOs kuwa wabunifu katika kutatua changamoto za wananchi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa mazingira, akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali na mashirika hayo ni muhimu katika kuhakikisha miradi inaleta matokeo chanya kwa wananchi wa Kilombero.

sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya

Mwenyekiti wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) Wilaya ya Kilombero, Benito Miwandu, akizungumza kwenye mkutano huo mjini Ifakara picha na Kuruthum Mkata

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) Wilaya ya Kilombero, Benito Miwandu, ameipongeza Serikali ya Wilaya kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa mashirika hayo. Hata hivyo, amesema bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutofahamika kwa mamlaka inayosimamia masuala ya NGOs na ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya maafisa maendeleo ya jamii.

Sauti ya Mwenyekiti wa NGOs Wilaya ya Kilombero,