Pambazuko FM Radio

Kimbiru Ulanga kupiga Vita Migogoro ya Wakulima na Wafugaji

9 November 2026, 17:09

Baadhi ya Wananchi wa Kimbiru Igota Wilayani Ulanga wakiwa kwenye mkutano wa Makubaliano Picha na Nicolatha Mpaka

Tumekubaliana faini ya Milioni Mbili kwa kosa la kulisha Mifugo kwenye Shamba la Mkulima, Milioni Moja itaingia kwenye mfuko wa Jamii Milioni Moja nyingine kwa Mwathirika-Wananchi

Na Nicolatha Mpaka

Wakazi wa Kitongoji cha Kimbiru Igota, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, wamekubaliana kushirikiana kulinda amani na kuzuia migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Makubaliano hayo yamefikiwa Novemba 9, 2026, katika kikao cha jadi, ambapo mfugaji atakayeharibu shamba la mkulima kwa kuingiza mifugo yake atatozwa faini ya shilingi milioni mbili. Kati ya fedha hizo, milioni moja itaingia kwenye mfuko wa jamii na milioni moja kulipwa kwa mkulima aliyeathirika.

sauti ya Baadhi ya Wananchi

Shigilo Mlasu Holela, , Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kimbiru Kijiji cha Igota Ulanga akizungumza wakati wa Makubaliano hayo picha na Nocolatha Mpaka

Akizungumza kuhusu makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Shigilo Mlasu Holela, amesema hatua hiyo inalenga kulinda amani na kuimarisha uhusiano kati ya wakulima na wafugaji. Amewataka viongozi wengine kuiga mfano huo katika kutafuta suluhu ya migogoro hiyo.

Inspekta Badru Mtambo, Mkuu wa Kituo cha Polisi Lupiro, Wilayani Ulanga akitilia mkazo kwenye makubaliano hayo Picha na Nicolatha Mpaka

Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo cha Polisi Lupiro, Inspekta Badru Mtambo, amewapongeza wananchi kwa kuweka taratibu zinazolenga kulinda amani. Amesema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na jamii kusimamia sheria na kuhakikisha amani inadumu.