Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
2 November 2026, 18:24

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nyange Halmashauri ya Ifakara Mji walioudhuria Mkutano wa Hadhara Picha na Kuruthum Mkata
nakuagiza Mkurugeni wa Mji kuhakikisha ndani ya Siku 14 maeneo yote ya kilimo na malisho yanapaswa kutumika kwa shughuli zilizokusudiwa -DC Kyobya
Na Kuruthum Mkata
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, amewataka wananchi walioingia katika maeneo yaliyotengwa kwa kilimo na malisho kuondoka mara moja, akisisitiza kuwa maeneo hayo hayapaswi kugeuzwa makazi.

Wakili Dunstan Kyobya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akizungumza na Wananachi wa Kijiji cha Nyange Hlmashauri ya Ifakara Mji Picha na Kuruthum Mkata
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Uliofanyika Kitongoji cha Mtukula, Kata ya Msolwa Station, Oktoba 29, 2026,Dc Kyobya amesema maeneo ya kilimo na malisho yanapaswa kutumika kwa shughuli zilizokusudiwa ambapo ametoa wiki mbili kwa Mkurugenzi kuhakikisha wavamizi wanaondolewa.
sauti ya DC Kyobya
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Rashid semgoya amewataka viongozi wa vijiji na kata kusimamia matumizi sahihi ya maeneo hayo ili kudhibiti migogoro.
sauti ya Kaimu DED

Mkuu wa Idara ya Kilimo, Dkt. Yuda Mgeni, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyange picha na Kuruthum Mkata
Naye Mkuu wa Idara ya Kilimo, Dkt. Yuda Mgeni, amesema maeneo yaliyotengwa na Serikali kwa kilimo na ufugaji yanapaswa kuheshimiwa. Ameeleza kuwa ongezeko la watu limechangia migogoro hiyo, huku akiahidi kuchukua hatua dhidi ya uvamizi wa mifugo.
sauti ya Mkuu wa Kilimo
Diwani wa Kata ya Msolwa Station ameeleza kuwa kata hiyo inakabiliwa na changamoto za ubovu wa barabara, kutokuwepo kwa barabara ya kuingia na kutoka pamoja na ukosefu wa daraja.
sauti ya Diwani
Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Mtukula wameeleza changamoto wanazokutana nazo, ikiwemo migogoro kati ya wakulima na wafugaji, na kuomba hatua za kudumu zichukuliwe kukabiliana na hali hiyo.