Pambazuko FM Radio

TAWIRI yahimiza maisha Jumuishi ya Binadamu na wanyama

24 October 2026, 08:46

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Basa Mchipa akizungumza kwenye Uhifadhi na Jamii picha na Henry Mwakifuna

 kuna umuhimu wa kulinda misitu na vyanzo vya maji, kutunza taka za vyakula katika maeneo salama na kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa nyani katika mazingira, ikiwemo kusaidia usambazaji wa mbegu za mimea kwa baadhi ya spishi–Mtafiti wa TAWIRI

Na Henry Mwakifuna

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Basa Mchipa , amesema maisha jumuishi kati ya binadamu na nyani yanawezekana kwa jamii kuelewa tabia za wanyama hao na kulinda makazi yao asilia.

Akizungumza na Pambazuko FM Kwenye Uhifadhi na Jamii amesema ukataji wa misitu na upanuzi wa mashamba huwafanya nyani kukaribia makazi ya watu na kuharibu mazao, hali inayoweza kusababisha migogoro.

Ametoa mwito kwa wananchi kulinda misitu na vyanzo vya maji, kutunza taka za vyakula na kushirikiana na maafisa wa wanyamapori ili kujenga mazingira ambayo binadamu na nyani wanaweza kuishi pamoja kwa usalama na manufaa ya uhifadhi.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kushirikiana na maafisa wa wanyamapori pale nyani wanaposababisha uharibifu wa mazao au kuhatarisha usalama wao, akieleza kuwa kulinda makazi asilia ni hatua muhimu katika kupunguza migogoro na kuhifadhi mazingira.

sauti ya Mtafiti