Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
25 November 2026, 19:30

Amesema mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa tangu mwaka 2023 na mkandarasi tayari amelipwa fedha za awali
Na Kuruthumu Mkata
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, amempa mkandarasi wa barabara ya Ifakara–Mbingu yenye urefu wa kilometa 62.5 siku 30 kuanza ujenzi, baada ya Serikali kumlipa fedha za awali za mradi huo.
Agizo hilo amelitoa Novemba 25, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule ya msingi Lukolongo, kata ya Mchombe Halmashauri ya Mlimba, akitaka ifikapo Desemba 25, mwaka huu, mitambo iwe imeanza kazi badala ya mkandarasi kuendelea kutembelea eneo la mradi bila utekelezaji.
Aidha, ameitaka Wizara ya Ujenzi kufuatilia mradi huo na kumpelekea taarifa pamoja na picha za maendeleo yake awali, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa mwaka 2023 na mkandarasi tayari amelipwa fedha za awali.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya,amesema barabara hiyo inajengwa kwa awamu, huku akieleza kuwa sehemu ya Ifakara–Mlimba tayari ina mkandarasi aliyelipwa zaidi ya shilingi bilioni tisa ili aanze kazi.
Ameielekeza Wizara kuhakikisha mkandarasi huyo anaanza ujenzi haraka iwezekanavyo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mlimba amesema barabara hiyo ni miongoni mwa kero kubwa zinazowakabili wananchi, akieleza kuwa ni kiungo muhimu cha kiuchumi kwa Mkoa wa Morogoro.
Amesema mkandarasi hajaanza kufanya kazi na kuiomba Serikali kuingilia kati ili kuhakikisha mradi unatekelezwa.

Wakati huo huo, baadhi ya wananchi wa Mlimba waliohudhuria mkutano huo wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, huku wakiiomba Serikali kuzitafutia ufumbuzi.
