Pambazuko FM Radio

Wenye Ulemavu wataka Elimu na Taarifa za Uhifadhi

10 October 2026, 10:17

changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu katika kupata taarifa na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi-Mosese Anthony Makereketa

Mosese Makereketa, mtu mwenye ulemavu wa Kijiji cha Mbingu, Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero akizungumza juuu ya masuala ya ushirikishwaji kwenye Uhifadhi picha na Henry Mwakifuna

Na Henry Mwakifuna

Mosese Anthony Makereketa, mtu mwenye ulemavu wa kutokuona kutoka Kijiji cha Mbingu, Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero, ameitaka jamii kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashirikishwa katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori.

Akizungumza na Pambazuko FM, Makereketa amesema kuwa kabla ya kupata ulemavu alikuwa akishiriki katika masuala ya uhifadhi, lakini baada ya kupata ulemavu amebaini changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu katika kupata taarifa na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi.

Mosese Makereketa, mtu mwenye ulemavu wa kutokuona kutoka Kijiji cha Mbingu, Halmashauri ya Mlimba akifanya mahojiano na Mwandishi wa Taarifa hiii picha na Mwakifuna

Amesisitiza kuwa watu wenye ulemavu wanapaswa kupata elimu na taarifa sahihi kuhusu uhifadhi ili waweze kushiriki katika kulinda mazingira na wanyamapori, badala ya kuachwa nyuma katika juhudi hizo.

sauti ya Mosese Makereketa