Pambazuko FM Radio

Wacheza Karate Bonde la Kilombero watakiwa kuungana

7 November 2026, 08:13

Jeremia Mapima maarufu Master Ngii akizungumza na Mwandishi wa Taarifa hiii picha na Mwakifuna

kucheza karate kiholela si jambo zuri tunahitaji kuungana wa Itete Malinyi Mlimba ifakara na Bonde lote la Kilombero-Master Ngii

Na Henry Mwakifuna

Master Ngii Jeremia Mapima amesisitiza umuhimu wa kuunda umoja wa wacheza karate katika Bonde la Kilombero badala ya kufanya mchezo huo kiholela.

Amesema karate ni mchezo unaosaidia kujenga afya bora, kuimarisha mwili na kuwapa wachezaji uwezo wa kujihami wanapokabiliwa na changamoto za kiusalama.

Ameongeza kuwa kuungana kwa wachezaji kutasaidia kuweka utaratibu mzuri wa mchezo huo na kuimarisha maendeleo ya karate katika Bonde la Kilombero.