Pambazuko FM Radio

Unyonyeshaji duni wahatarisha ukuaji wa watoto-Ifakara

24 November 2026, 20:10

Picha ya baadhi ya Wazazi wakipatiwa huduma ya Kliniki Kijiji cha Mpofu-Mlimba(Picha na Katalina Liombechi)

Hali hiyo inaweza kuathiri uzalishaji wa maziwa ya mama na kuathiri unyonyeshaji

Na Katalina Liombechi

Tabia ya baadhi ya wazazi kupunguza kiwango cha chakula wanachokula kwa lengo la kurejesha maumbo yao ya awali kabla ya kumaliza kipindi kinachoshauriwa cha kunyonyesha imeelezwa kuwa hatari kwa afya na ukuaji wa watoto kimwili na kiakili.

Akizungumza na Pambazuko FM, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bi Lidya Kikoga amesema tabia hiyo imekuwa ikichochewa na baadhi ya wazazi kuiga maisha ya watu maarufu na kutaka kurejesha maumbo yao haraka.

Amesema hali hiyo inaweza kuathiri uzalishaji wa maziwa ya mama na kuathiri unyonyeshaji, huku akiwataka wazazi kuzingatia elimu wanayopewa kliniki na kuepuka kujinyima chakula wakati wa kunyonyesha.

Picha ya Lidya Kikoga Afisa lishe Halmashauri ya mji wa Ifakara(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Lidya Kikoga Afisa lishe

Aidha, amesema Halmashauri inaendelea kuweka mikakati ya kutoa elimu ya lishe bora na kuhamasisha uzingatiaji wa kanuni za unyonyeshaji kwa vitendo, kuanzia ngazi za vijiji, ili kuhakikisha watoto wanapata malezi na lishe stahiki.

Sauti ya Afisa lishe 2

Kwa upande wao, baadhi ya wazazi wamesema elimu wanayoipata katika vituo vya afya imekuwa msaada mkubwa katika kuimarisha uelewa wao kuhusu unyonyeshaji Wamewataka wazazi wenzao kuepuka tabia ya kujinyima chakula kwa ajili ya kurejesha maumbo yao na badala yake kuweka mbele afya na ustawi wa watoto.

Picha ya baadhi ya wazazi Kijiji cha Mpofu Mlimba wakipatiwa elimu kupitia huduma ya kliniki(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti za baadhi ya wazazi