Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
16 October 2026, 12:30

Hashim Mwangongonyongo, Mwalimu wa Hisabati na TEHAMA katika Shule ya Msingi Lupa Ifakara akizungunza na Pambazuko FM, Picha na Henry Mwakifuna
Nimelazimika kutoa elimu hii ili kuwarahisishia Watumiaji na wafanya biashara waweze kujua mwenendo wa shughuli zao-Mwalimu wa TEHAMA.
Na Henry Mwakifuna
Jamii ya Ifakara imetakiwa kutumia mifumo ya TEHAMA katika kufuatilia shughuli za biashara ili kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu, kujua faida na hasara pamoja na kutathmini mwenendo wa biashara zao.
Akizungumza na Pambazuko FM, Hashim Mwangongonyongo, Mwalimu wa Hisabati na TEHAMA katika Shule ya Msingi Lupa, Ifakara, amesema mifumo hiyo humsaidia mfanyabiashara kufuatilia utendaji wa biashara kwa siku, wiki au mwezi, kupitia ripoti zinazomuwezesha kufanya maamuzi sahihi na kudhibiti matumizi.
Amesema baadhi ya mifumo hutumia mtandao wa intaneti, huku mingine ikiweza kufanya kazi bila mtandao, kulingana na mahitaji ya biashara husika.
Hata hivyo, matumizi ya mifumo hiyo bado hayajaenea kwa wafanyabiashara wengi katika jamii ya Ifakara, hali inayoweza kufanya baadhi yao kushindwa kutambua kwa usahihi mwenendo wa biashara zao kutokana na changamoto za utunzaji wa kumbukumbu.
Hivyo, jamii imetakiwa kuongeza uelewa na matumizi ya mifumo ya TEHAMA ili kuimarisha usimamizi wa biashara na kuongeza ufanisi katika shughuli za kiuchumi.
sauti ya Mwalimu wa TEHAMA