Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
12 November 2026, 12:41

Wakili Dunstan Kyobya, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akisisitiza Jambo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mlimba picha na Henry Mwakifuna
Hakuna eneo la Wafugaji bali eneo la Malisho ambalo halipaswi kujengwa Makazi ya Wafugaji ni malisho tu-DC Kyobya
Na Henry Mwakifuna
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, amewataka madiwani wote kuhakikisha wanatambua na kuainisha maeneo ya matumizi bora ya ardhi katika kata zao ili kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji.
Amesema maeneo ya malisho ni maalumu kwa ajili ya mifugo na hayapaswi kutumiwa na wafugaji kujenga makazi.
Aidha, ameeleza kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwaruhusu wafugaji kuingia katika maeneo mbalimbali bila kufuata taratibu zilizowekwa.
Kyobya ameyasema hayo wakati akizungumza katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mlimba.
Sauti ya DC Kyobya