Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
30 September 2026, 15:20
Katika kipindi hiki cha wiki moja tutakuwa tukitoa huduma mbalimbali za ardhi na kushughulikia migogoro inayohusiana na ardhi, ikiwemo migogoro ya vijiji na taasisi zilizopo katika eneo hili.” Rajabu Bogwa

Baadhi ya Wataalam wa Ardhi wa Halmashauri ya Ifakara Mji wakitoa Huduma kwa Wakazi wa Kata ya Kidatu Picja na Henry Mwakifuna
Na Henry Mwakifuna
Zaidi ya wananchi 1,000 katika Kata ya Kidatu, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Wilayani Kilombero wanatarajiwa kunufaika na huduma zinazotolewa kupitia Kliniki ya Ardhi, iliyoanza kutolewa Septemba 28 na inatarajiwa kuendelea kwa kipindi cha wiki moja.
Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Rajabu Bogwa, ameiambia Pambazuko FM kuwa kliniki hiyo inalenga kuwafikishia wananchi huduma za ardhi kwa urahisi, pamoja na kusaidia kutatua migogoro mbalimbali inayohusiana na ardhi katika eneo hilo.

Mkuu wa Idara ya Ardhi kutoka Halmashauri ya Mji wa Ifakara akisikiliza kwa Umakini wakati akizungumza na Pambazuko FM Picha na Henry Mwakifuna
Bogwa amesema wananchi wenye changamoto au migogoro ya ardhi wanapaswa kutumia fursa hiyo kufika katika kliniki hiyo ili kupata huduma na ushauri kutoka kwa wataalamu wa Idara ya Ardhi.
Kliniki hiyo imeanza kutolewa Septemba 28 katika Kata ya Kidatu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Halmashauri ya Mji wa Ifakara kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi na kusaidia kushughulikia changamoto zinazohusiana na ardhi.
sauti ya Mkuu wa Idara ya Atdhi Rajabu Bogwa