Jamii FM

Shekhe Mkuu Mtwara aiomba jamii kutatua kero ya maji sekondari ya Mkanaledi

21 February 2025, 14:42 pm

Shehe mkuu wa mkoa wa Mtwara ,Shehe Jamaldin akipata maelekezo juu ya utendaji kazi wa Zahanati ya Magomeni Manispaa ya Mtwara Mikindani (Picha na Musa Mtepa)

Hii ilikuwa ziara ya kawaida kwa Shehe mkuu wa mkoa wa Mtwara kutembelea katika miradi mbalimbali ya kijamii na kuongea na jamii juu ya umuhimu wa mshikamano,kutii viongozi na mamlaka kama dini ya kiislamu inavyoelekeza.

Na Musa Mtepa

Jamii na wadau wa maendeleo mkoani Mtwara wametakiwa kushirikiana kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika shule ya sekondari Mkanaledi, kwa kusaidia uchimbaji wa kisima ili kuondoa mzigo wa bili za maji kila mwezi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya elimu, afya na dini, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Shekhe Jamaldin Salim Chamwi, amesema kuwa shule ina zaidi ya wanafunzi 380, na kwamba maji yaliyopo kwa sasa hayatoshi.

Amehimiza jamii na wadau wa maendeleo kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa kwa kuchimba kisima, hivyo kuondoa adha ya kulipia bili za maji kila mwezi.

Sauti ya Shekhe Jamaldini Chamwi shekhe mkuu wa mkoa wa Mtwara.

Pia, Shekhe Chamwi ameomba jamii kuchangia na kumaliza ujenzi wa Masjid Muzdalifa unaoendelea kujengwa katika kata ya Magomeni, Manispaa ya Mtwara Mikindani, akisisitiza umuhimu wa mshikamano na umoja katika jamii kwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Sauti ya 2 Shekhe Jamaldini Chamwi shekhe mkuu wa mkoa wa Mtwara.

Mjumbe wa Baraza la Mashehe Mkoa wa Mtwara, Shehe Mohmedi Salim Lidonge, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Maridhiano na Amani Tanzania Mkoa wa Mtwara, amesisitiza kuwa serikali imefanya kazi kubwa katika ujenzi wa shule ya sekondari, na sasa ni jukumu la jamii kujitolea kumaliza changamoto ya maji.

Aidha ameonesha masikitiko kutokana na ukamilikaji wa ujenzi wa masjid Muzdalifa kutokamilika kwa wakati kutokana na kukosekana kwa fedha za kumalizia.

Sauti ya Shehe Mohamed Lidonje mjumbe wa Baraza la mashehe mkoa wa Mtwara.

Shehe Abdulhafidhi Kilindi, Shehe Mkuu wa Kata ya Magomeni, ameelezea faida ya ziara hiyo akisema imekuwa na manufaa makubwa kwani imeweza kuona changamoto mbalimbali zinazohitaji ufumbuzi katika miradi iliyotembelewa.

Sauti ya Shehe Abdulhafidhi Kilindi shehe mkuu kata ya Magomeni

Ziara hii ni sehemu ya juhudi za kuhimiza mshikamano, utendaji kazi bora, na utii kwa viongozi, ikiwa ni moja ya mafundisho ya dini ya Kiislamu.