Mpanda FM
Mpanda FM
16 July 2025, 4:04 pm

Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Mpanda Anyulumye Longo. Picha na Leah Kamala
“Usipompa mtoto haki yake ya elimu ni rahisi kujiingiza kwenye makundi hatarishi”
Na Leah Kamala
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuwafundisha maadili mema watoto na kuwapatiwa haki yao ya elimu ili kujiepusha na makundi yasiyofaa.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa wanawajibika vyema kuhakikisha watoto wanapata elimu bora ili kuboresha maisha yao na jamii nzima.
Nae Afisa ustawi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Anyulumye Longo amewashauri wazazi na walezi kushirikiana na walimu na kutoa mahitaji muhimu ya shule kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya watoto wao.
Elimu ni hazina kubwa kwa wanafunzi kwani huwajengea msingi wa maisha bora na kutimiza ndoto zao ili kufikia mafanikio ya baadae.