Mpanda FM

Wazazi, walezi wahimizwa kuzingatia chanjo ya polio

16 April 2025, 1:29 pm

Picha ya mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph. Picha na Anna Mhina

” Wazazi na walezi hakikisheni mnazingatia tarehe ya chanjo ya polio”

Na Edda Enock

Wazazi na walezi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia kikamilifu chanjo kwa watoto ili kujikinga dhidi na ugonjwa wa polio.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ambae alikuwa mwenyekiti katika kikao cha Taarifa ya utekelezaji wa lishe kwa nusu mwaka julai-Desember 2024 kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Christina Bunini amewataka viongozi mbali mbali kuendelea kutoa Elimu juu ya umuhimu wa chanjo kwa wananchi hasa kwa wanawake wajawazito.

Sauti ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo

Nae Sophia Kumbuli mkurugenzi manispaa ya Mpanda amewataka viongozi kuhakikisha wanahamasisha wananchi kuhusiana  lishe ,chanjo pamoja na usafi wa mazingira.

Sauti ya mkurugenzi manispaa ya Mpanda

Kikao hicho kilikua kimelenga kutekeleza shughuli mbambali za lishe kwa lengo la kuimarisha afya na hali ya lishe katika jamii.