Mkuu wa Mkoa Katavi Awaonya Viongozi Kuhusu Uhalifu
20 November 2021, 11:45 am
Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka viongozi wa serikali kutokuwa chanzo cha kukumbatia uharifu katika jamii.
Akizungumza na Mpanda Radio Fm amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya viongozi wa serikali kutumia nafasi zao za kazi kuwatetea waharifu pindi wanapokuwa wametiwa hatiani.
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi ACP Benjamini Kuzaga amesema ulinzi wa raia na mali zake sio jukumu la polisi peke ake bali ni wajibu wa kila mtu huku akiwataka baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa kuacha tabia ya kuwaficha waharifu katika maeneo yao.
Sambamba na hilo Kuzaga ameeleza kuwa Jeshi la polisi limekuwa likijitahidi kudhibiti matukio ya kiharifu licha ya kutopewa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wananchi na viongozi wa mitaa