Mpanda FM
Huduma Mkoba Kuimarisha Zoezi la Chanjo ya Uviko 19
20 November 2021, 11:35 am
Serikali mkoani katavi imekuja na mpango harakishi na shirikishi wa kutoa huduma mkoba ya uviko19 ambavyo itawasaidia wananchi kupata chanjo hiyo popote pale walipo.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkao wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ambapo ameeleza kuwa wamekuja na huduma hiyo katika kuhakikisha wananchi walio mbali na vituo vya afya wananpata chanjo hiyo.
Aidha Mrindoko amesema kuwa vituo vya kutolea huduma ya chanjo ya uviko 19 vimeongezeka kutoka vituo 45 hadi 86.
Hata hivyo mrindoko ameomba wananchi kupuuza maneno yote yanatolewa na watu yakilenga kupotosha jamii kuhusu chanjo ya uviko 19 huku akitanabaisha kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na wataalam wa afya.