Bilioni Nne Kunufaisha Halmashauri ya Nsimbo
19 November 2021, 10:29 am
Halmashauri ya Nsimbo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imepata zaidi ya shiling bilioni nne kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo vyumba vya madarasa.
Akizungumza na kituo hiki mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mohamed Ramadhani amesema kuwa kupatikana fedha hizo ni neema kubwa kwa halmashauri hiyo kwani itasaidia kupunguza baadhi ya changamoto ikiwemo kuongezeka kwa vyumba vya madarasa
Aidha Ramadhani amewataka wananchi katika halmashauri hiyo kuendelea kuziunga mkono kwa vitendo juhudi zinazoonyeshwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa walinzi juu ya watu wenye lengo baya juu ya miradi hiyo
Halmashauri ya nsimbo ni miongoni mwa Halmashauri za manispaa ya mpanda mkoani katavi zilizo pokea fedha zaidi ya bilioni nne zilizotolewa na serikali kutoka benki ya dunia