Wazee Uwanja wa Ndege Waonya Vikundi Vya Uhalifu
19 November 2021, 12:23 pm
Wazee wa kata ya uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamewashauri wazazi na walezi katika kata hiyo kuwaeleza watoto juu ya madhara yatokanayo na kujihusisha na makundi ya kiuharifu
Wakizungumza na kituo hiki mara baada ya kikao na diwani wa kata hiyo Maiko Kamande Mbogo wazee hao wamesema ili kata hiyo isiwe na makundi ya watoto wenye tabia za udokozi na vitendo vingine vya uharifu ni lazima wazazi kuwajibika ipasavyo
Kwaupande wake diwani Maiko Kamande Mbogo akizungumza juu ya baadhi ya watoto kushiriki katika makundi ya kiuharifu amesema kuwa inatokana na baadhi ya wazazi na walezi kujisahau wajibu wao.
Kata ya uwanja wa ndege inajumla ya mitaa mitatu ambayo ni Mtaa wa msufini ,mtaa wa Airtel na mtaa wa mnazi mmoja.