Jamii FM

Waziri Dkt. Stergomena Tax Azindua  Shule ya Msingi Chawi Mkoani Mtwara

8 October 2024, 13:05 pm

Mradi huo unaojumuisha Vyumba 9 vya Madarasa, Jengo la Utawala pamoja Matundu 6 ya Vyoo, umetekelezwa kwa fedha zilizotoka Serikali kuu.

Na Musa Mtepa

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax, amefanya ukaguzi na kufungua mradi wa Shule ya Msingi Chawi, iliyopo Kijiji cha Chawi, Halmashauri ya Mji Nanyamba, mkoani Mtwara wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara baada ya uzinduzi wa mradi huo tarehe 7 Oktoba 2024, Dkt. Tax amesema kuwa kuwepo kwa miradi mingi inayoendelea kutekelezwa Mtwara tayari imeshafunguka.

Aidha ameongeza kwamba katika kipindi cha miaka mitatu, mkoa wa Mtwara umepokea zaidi ya shilingi bilioni 700 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Sauti ya Stergomena Tax Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, ameeleza kwamba Halmashauri ya Mji Nanyamba ni miongoni mwa wafaidika wakubwa wa miradi ya kimkakati inayotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sauti ya Kanal Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara.

Muhandisi Mshamu Munde, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, amefafanua kuwa  hapo awali shule hiyo ilikuwa na hali ambaya ya kimiundombinu hali iliyopelekea mwaka 2022 kufanyika uhakiki na kugundua shule hiyo kuwa na changamoto kubwa ndipo walipopeleka fedha na kuanza ujenzi wa vyumba  vya madarasa vyenye uwezo wa kuchukua Watoto zaidi ya 500.

Sauti ya Muhandis Mshamu Munde mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Mji Nanyamba.

Ujenzi wa majengo haya umegeuza shule hiyo kuwa kivutio, ambapo watoto wanatamani kuendelea na masomo, tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali.