Jamii FM

Waziri wa Ulinzi kukagua miradi ya maendeleo Mtwara DC

5 October 2024, 08:34 am

vyumba vya madarasa vya shule ya sekondari Mustafa Sabodo ni moja ya miradi itakayotembelewa na waziri wa ulinzi(picha na Musa Mtepa)

Waziri wa ulinzi ataanza ziara Oktoba 6, 2024 katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara ambapo ataanza na ukaguzi wa vyumbo vya madarasa vilivyopo katika shule ya sekondari Mustafa Sabodo na kumalizia uwekaji wa jiwe la msingi nyumba ya Watumishi wa afya katika Zahanati ya Kijiji cha Likonde.

Na Musa Mtepa

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara vijijini Abeid Abeid Kafunda amewaomba wananchi kujitokeza kwa uwingi October 6,2024 katika ziara ya  Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa Dkt Stergomena Lawrence Tax atakapotembelea miadi ya maendeleo ambapo ataweka  jiwe la msingi na kuzinduzi vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Sabodo .

Akizungumza October 4, 2024 baada ya kamati ya ukaguzi ya mkoa  kutembelea na kukagua miradi hiyo Kafunda amesema wanamtwara hawana budi kujitokeza   kwa uwingi kwa kumsikiliza na kushukrani za dhati kwa  Rais Dkt Samia Suluhu Hassani   kwa mambo anayoendelea kuwafanyia katika halmashauri ya Mtwara.

Sauti ya Abeid Abeid Kafunda Mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara dc
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara dc Abeid Kafunda akielezea ziara ya waziri wa ulinzi katika halmashauri yake(picha na Musa Mtepa)

Aidha Kafunda ameelezea miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na kamati hiyo kuwa ni Pamoja na mradi wa madarasa mawili,ofisi moja ya walimu ,matundu 6 ya vyoo katika shule ya Sekondari Mustafa Sabodo na mradi wa nyumba ya watumishi iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Dangote kupitia CSR.

Sauti ya 2 Abeid Abeid Kafunda mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara dc
Nyumba ya watumishi wa afya katika zahanati ya Likonde iliyojengwa kwa kampuni ya Dangote kupitia CSR(Picha na Musa Mtepa)

Ni zaidi ya Milioni 206 imefanikisha ujenzi wa miradi hiyo ambapo milioni 56 imefanikisha ujenzi wa madarasa mawili,ofisi moja ya walimu ,matundu 6 ya vyoo katika shule ya Sekondari Mustafa Sabodo na shilingi milioni 156 itafanikisha ujenzi wa nyumba ya watumishi wa afya katika Kijiji cha Likonde ,kata ya Mayanga Mtwara Dc.