Mpanda FM

Recent posts

1 February 2023, 11:51 am

Mrindoko Atoa Siku Saba Majibu ya Mkataba wa Lishe

KATAVIMkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametoa siku saba kwa wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu walaya na maafisa lishe kutoa maelezo ya kina kwa maandishi kwa kushindwa kusimamia mkataba wa lishe. Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao cha kujadili…

25 January 2023, 10:44 am

Zaidi ya Miti Millioni Mbili Inataraji Kupandwa Tanganyika

MPANDAJumla ya miti milioni mbili na elfu kumi na nne inatarajiwa kupandwa katika maeneo mbalimbali wilayani Tanganyika mkoani katavi. Hayo yamesemwa na Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya mpanda Jamila Yusufu wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji…

21 January 2023, 8:34 pm

Fahamu Matumizi Sahihi ya Alama za Zebra

MPANDAMadereva wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya vivuko vya barabara ili kuepusha ajali ambazo zinatokea katika vivuko . Hayo yamesemwa na mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Geofrey Braiton, kuwa ni sheria kwa…

20 January 2023, 4:11 am

Wakazi wa Ibindi Walia na Barabara

NSIMBO Wananchi wa kijiji cha ibindi kata ya Ibindi Halmshauri ya Nsimbo  Mkoani Katavi wameuomba uongozi wa kata hiyo kuboresha miundombinu ya barabara ambayo wametaja kama kikwazo katika shughuli za kimaendeleo. Wakizungumza na Mpanda redio fm wananchi hao wamesema barabara…

20 January 2023, 3:57 am

Madereva Bajaji Walia na Bima

KATAVI Baadhi ya madereva bajaji mkoani Katavi wameeleza namna ambavyo bima za vyombo vya moto haziwasaidii pindi yanapotokea majanga ya barabarani. Wameyaeleza hayo wakati wakipewa elimu juu ya umuhimu wa bima za vyombo vyao vya moto ambapo wamesema aina hiyo…

20 January 2023, 3:53 am

Wananchi Kabungu Wadai Mkunga wa Kike

TANGANYIKABaadhi ya wananchi wa kijiji cha Kabungu kata ya Kabungu wilayani Tanganyika mkoani katavi wameiomba Serikali kuwaletea mkunga wa kike kwenye zahanati ya kijijini hapo.Wakizungumza na mpanda radio fm wananchi hao wameipongeza zahanati hiyo kwa huduma wanazozitoa huku wakiomba waongezewe…

20 January 2023, 3:18 am

Katavi Bila Malaria Inawezekana

MPANDA Ili kujikinga na ugonjwa wa Malaria wananchi manispaa ya mpanda mkoani katavi wameshauriwa kutokomeza maeneo yote ambayo yanaweza kuwa ni chanzo cha mazalia ya mbu sambamba na kutumia chandarua wakati wa kulala. Ushauri huo umetolewa na mganga mkuu manispaa…

20 January 2023, 3:14 am

Uzinduzi wa Jengo la Mahakama Katavi

KATAVI Watumishi wa Mahakama nchini wametakiwa kutenda haki na kuepuka vitendo vya rushwa ili kuwahudumia wananchi kwa haki,usawa na kwa wakati. Hayo yamesemwa na Jaji Kiongozi Mahakama Kuu Tanzania Mustapher Mohamed Siyani wakati akizungumza katika uzinduzi wa mahakama za hakimu…

17 January 2023, 6:04 pm

Magari ya Shule Kubeba Wanafunzi Kuliko Uwezo.

MPANDA Kutokana na kuendelea kukithiri kwa changamoto ya magari ya shule kubeba wanafunzi idadi kubwa kuliko uwezo, wananchi mkoani Katavi wamewataka wamiliki wa shule kuzingatia sheria zinavowataka. Wakizungumza na mpanda radio fm wananchi wamesema kuwa wameshuhudia baadhi ya magari hayo…

17 January 2023, 5:49 pm

Kilio Watendaji Uuzaji Pombe Muda wa Kazi

MPANDA Baadhi ya wananchi Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema kuwa kuendelea kuwepo kwa wafanyabiashara wanaofungua kumbi za starehe na pombe kinyume na muda uliopangwa unachangiwa na watendaji wasio wajibika katika usimamizi wa sheria Wakizungumza na mpanda radio fm wananchi…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.