Mpanda FM
Mpanda FM
9 January 2025, 9:31 am
“Kuweka malengo mwanzoni mwa mwaka husaidia kuepuka matumizi yasiyoyalazima“ Na Lilian Vicent -Katavi Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi wamesema kuwa kuweka malengo mwanzoni mwa mwaka ni moja ya sababu inayochangia kufikia mafanikio kwa wakati. Wakizungumza na Mpanda Redio FM wamebainisha…
8 January 2025, 8:43 pm
“changamoto ambazo zinapelekea mradi huo kuchelewa kukamilika ikiwemo upatikanaji wa wadhabuni kwa vifaa“ Na John Benjamin -Katavi Kamati ya kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi haijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule ya sekondari…
8 January 2025, 12:24 pm
“Amewataka wauguzi na wananchi kutumia gari hilo kwa kufuata kanuni sheria na miongozo ya serikali” Na Rachel Ezekia-Katavi Mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Lupembe amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Itenka Kilichopo hlmashauri ya Nsimbo Wilayani…
7 January 2025, 6:34 pm
“Kata ya Mpanda Hotel hakuna mtu mwenye ulemavu ambae amenufaika na TASAF “ Na Samwel Mbugi-Katavi Katibu wa chama cha watu wenye ulemavu mkoa wa Katavi Godfrey Albeto Sadala amesema watu wenye ulemavu wanabaguliwa kuingizwa kwenye mradi wa wanufaika wa…
6 January 2025, 7:18 pm
“Ameutaka uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kulipa fidia ya mbegu kama sehemu ya uharibifu” Na Samwel Mbugi -Katavi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya kuhakikisha doria zinazofanyika katika misitu na…
3 January 2025, 10:21 pm
“wao kama viongozi wa CHADEMA watahakikisha wanamuunga mkono Tundu Lissu kwa ajili ya maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla.“ Na Edda Enock-Katavi Viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Katavi Wamemuunga mkono Tundu Lissu Katika kuwania…
3 January 2025, 10:05 pm
“wazazi hakikisheni mnatunza fedha kwa ajili ya kuwanunulia watoto nguo za sikukuu ili kuwaepushia watoto msongo wa mawazo“ Mtoto mwenye umri wa miaka 8 amefariki dunia mkoani Katavi mara baada ya kujinyonga kutokana na kukosa nguo za sikukuu Akizungumza na…
3 January 2025, 9:34 pm
“kipindi cha mwaka 2024, jeshi la polisi mkoa wa Katavi limefanikiwa kudhibiti wizi wa mifugo ambapo watuhumiwa 48, walikamatwa kwa kosa la wizi wa mifugo“ Na Leah Kamala-Katavi Jeshi la polisi mkoa wa katavi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 8064 kwa kipindi…
1 January 2025, 9:04 pm
“kupitia sera ya utawala bora wamejipanga kutambua makundi ya watu wenye ulemavu kwani wamekuwa wakisahaulika katika jamii“ Na Samwel Mbugi – Katavi Baadhi ya watu wenye ulemavu Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameshiriki chakula cha pamoja…
31 December 2024, 10:14 pm
“wameguswa kutoa msaada kwa watu hao wenye uhitaji kuliko kwenda kufanya starehe “ Na Samwel Mbugi-Katavi Baadhi ya wanawake katika wodi ya wazazi pamoja na watoto yatima wanaoishi kituo cha mtakatifu Yohane Poul wa II Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi…
Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.
Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.
Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.
Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.
