Mpanda FM

Gabriel “Zingatieni kanuni za afya kuepuka kipindupindu”

27 March 2026, 1:36 pm

Picha na Roda Elias

“Tunaomba tupatiwe elimu maana hatuna uelewa”

Na Roda Elias

Wananchi wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameomba kupatiwa elimu juu ya ugonjwa wa kipindu pindu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa ili kuepuka mlipuko wa ugonjwa huo.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi wamesema  ugonjwa huo  unasababishwa na mchafuko wa hewa, na mazingira kuwa machafu huku wakiiomba serikali kuwapatia elimu juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Sauti za wananchi

Kwa upande wake daktari Gabriel Elias ameeleza  kuwa mara mtu anapopatwa ugonjwa huo dalili zake huanza kuonekana ndani ya siku mbili ,hivyo  mgonjwa  anapaswa kuwahishwa kituo cha afya kwa ajili ya matibabu.

Sauti ya daktari

Katika hatua nyingine  Gabriel ameiasa jamii kuzingatia kanuni za afya  ili kuepukana   na kujikinga na ugonjwa huo.

Sauti ya daktari

 Kwa  mujibu wa European Centre for Disease Prevention and Control {ECDC} hadi kufikia Februari 2026 kumeripotiwa visa 25,000 na vifo 280 vilivyoripotiwa vya ugonjwa wa kipindupindu.