Mpanda FM
Mpanda FM
27 March 2026, 12:47 pm

“Tunapewa mikopo bila elimu”
Na John Benjamin
Kutokutolewa kwa elimu ya mikopo kwa baadhi ya taasisi za kifedha imetajwa kuwa moja ya sababu ya baadhi ya wananchi mkoani Katavi kushindwa kufanya marejesho ya mikopo.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wamekuwa wakienda kukopa katika tasisi za kifedha zinazotoa pia mikopo kulingana na shida zao na kueleza kuwa hakuna elimu yoyote ya matumizi ya fedha wanayopatiwa pindi wanapohitaji kukopa.
Kwa upande wake Meneja msaidizi idara ya mawasiliano kutoka Benki kuu ya Tanzania Noves Moses amesema kuwa taasisi zote za kifedha zinazojishughulisha pia na utoaji wa mikopo zinawajibu wa kutoa elimu kabla kwa mwananchi anayehitaji kupatiwa mkopo huku akiwataka wananchi kufanyia kazi fedha wanayopatiwa.
Hivi karibuni naibu waziri wa fedha na mipango na mbunge wa jimbo la Kavuu Laurent Luswetula akiwa mkoani Katavi amesema kuwa wizara inaendelea kutoa elimu ya mikopo kwa wananchi.