Mpanda FM

Sheria zinavyomlinda mtoto wa kufikia

23 March 2026, 2:17 pm

Sweetbeth Nkumpilo wakili wa kujitegemea Mpanda. Picha na Anna Mhina

“Sheria inakataza kumnyanyasa ama kumbagua mtoto”

Na Anna Mhina

Wazazi na walezi wilayani Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kutambua jukumu lao katika kuwapa malezi bora watoto bila ubaguzi.

Wito huo umekuja kutokana na  jamii kuendelea kukumbwa na matukio ya baadhi ya wazazi na walezi kuwanyanyasa watoto wa kufikia kwa kutowapa haki zao na kuwafanyia vitendo vya ukatili wa kimwili pamoja na ubaguzi unaotokana na kutokuwa na uhusiano wa damu kati ya mzazi na mtoto.

Akizungumza na Mpanda redio FM wakili wa kujitegemea Sweetbeth Nkumpilo amesema sheria zipo wazi kulinda haki za mtoto bila kujali uhusiano wake na mlezi na kuongeza kuwa mtoto wa kufikia anastahili ulinzi sawa na mtoto wa kumzaa.

Sauti ya wakili

Kwa upande wao baadhi ya wazazi na walezi wameeleza sababu zinazopelekea kuwanyanyasa watoto wa kufikia ikiwa ni pamoja na visasi vya ndoa kuvielekeza kwa mtoto sambamba na wivu wa kurithi mali.

sauti za wananchi