Mpanda FM

Sumry awang’ata sikio vijana Mpanda

4 March 2026, 5:32 pm

Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Haidary Sumry akizungumza na vijana UVCCM Mpanda

Ameahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika katika kuhakikisha chama kinaimarika.

Na Samwel Mbugi-Katavi

Mbunge wa Jimbo la Mpanda mjini Haidary Hemed Sumry amekutana na baraza la umoja wa vijana CCM wilaya ya Mpanda kuwashukuru kutokana na namna wanavyoshiriki kuhakikisha chama kinakuwa imara.

Akizungumza katika kikao hicho amesema kushirikiana ndio nguzo peke inayoweza kuimarisha uhai wa chama na kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Haidary Sumry

Kwa upande wake mwenyekiti wa vijana wilaya ya Mpanda Joseph Ngoma amemshukuru mbunge kwa kuanza vizuri na jumuiya za chama na ameahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika katika kuhakikisha chama kinaimalika.

Sauti ya mwenyekiti wa vijana wilaya ya Mpanda Joseph Ngoma

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda Mussa Mwevi amewataka vijana kujivunia kumpata mbunge kijana anayetokana na umoja wa vijana.

Sauti ya Katibu wa CCM wilaya ya Mpanda

Hata hivyo Mwevi amewataka vijana kutoa ushirikiano katika maeneo yao pindi atakapo kuwa ziara za kufanya maendeleo katika maeneo yaliyopo ndani ya jimbo la Mpanda mjini.