Mpanda FM
Mpanda FM
27 February 2026, 4:41 pm

“Nimesikitishwa na uharibifu huu wa miundombinu, ulinzi ni lazima uwepo katika maeneo hayo”
Na Anna Milanzi-Katavi
Jumla ya madirisha 120 ya alminium yameibiwa katika shule za msingi, sekondari pamoja na zahanati zilizopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi
Hayo yameelezwa wakati wa kuwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka 2026-2027 pamoja na kufanya mapitio ya bajeti zilizopita miaka ya fedha ya hivi karibuni kwa halmashauri ya Nsimbo pamoja na manispaa ya Mpanda ambapo kwa manispaa ya Mpanda Leonard Kilamhama ambaye ni mchumi manispaa ya Mpanda amewasilisha kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda na kuainisha wizi huo.
Miongoni mwa wajumbe waliokowemo katika kikao hicho ni pamoja na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha maliki, amesikitishwa na vitendo hivyo na kuomba ulinzi kuhimarishwa katika miundombinu.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ameielekeza kamati ya usalama kuchukua hatua zaidi juu ya jambo hilo.

Kadhalika na hilo mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amepongeza ongezeko la bajeti kwa kila halmashauri ambapo halmashauri ya wilaya ya Nsimbo katika bajeti iliyopita ilikuwa ni billion 27.4 na kwasasa ni billion 35.7 huku manispaa ya Mpanda bajeti iliyopita ni Bilioni 33.9 kwa sasa ni Bilion 35.2 amesisitiza bajeti zote hizo zimelenga maendeleo kwa wananchi kama ambavyo serikali inasisitiza.