Mpanda FM

NEEMA KATAVI:Kaya masikini zapata bima ya afya

26 February 2026, 4:03 pm

Afisa uandikishaji NHIF akimuonesha kadi yake mmoja wa wanufaika. Picha na Betord Chove

“Msikubali kupitwa nafursa ya bima ya afya”

Na Betord Chove

Watu wapatao 23,236 kutoka kaya masikini  wanatarajia kunufaika na huduma ya bima kwa afya kwa wote kupitia mfuko wa TASAF mkoani Katavi.

Akitoa taarifa wakati wa hafla ya  uzinduzi wa  bima ya afya kwa wote kwa wanaolipiwa na serikali mkoani Katavi Meneja wa NHIF Ally Mwakababu amesema Mpanda manispaa waliondikishwa ni 1560, Nsimbo 1774, Mpimbwe 1151, Mlele 303, Tanganyika 1172, huku changamoto kadhaa zikijitokeza wakati zoezi hilo likiendelea.

Sauti ya meneja wa NHIF

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wanufaika wote wa awamu ya kwanza kuhakikisha wanasajiliwa ili waweze kunufaika na bima ya afya kwa wote.

Mkuu wa mkoa wa Katavi akimkabidhi kadi ya bima ya afya mmoja wa wanufaika.
Sauti ya mkuu wa mkoa

Kwa upande wa wanufaika waliofanikiwa kujiandikisha na kupata bima  hizo awamu ya kwanza wameishikuru serikali kwa kuwapa huduma hiyo ambayo awali ilikuwa changamoto kutokana na ugumu wa maisha.

Sauti za wanufaika

Awamu ya kwanza ya uandikishaji wa bima ya afya kwa wote nchini inatarajiwa kuwasajili wanufaika milioni moja laki moja na ishirini na tano mia tatu thelathini {1,125330} ambao ni wazee, watoto , mama wajawazito,  watu wenye ulemavu na watu wenye mahitaji maalumu waliotambuliwa na TASAF.

.