Mpanda FM

Usafi wa kinywa kwa watoto, fumbo kwa wazazi

21 February 2026, 7:19 pm

picha na mtandao

Wanatumia vitambaa na wengine kutumia mikono pasipo kujua njia sahihi za kitaalamu kwa ajili ya kusafisha vinywa vya watoto.

Na Rhoda Elias-Katavi

Baadhi ya wananchi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameeleza kuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya namna sahihi ya kusafisha vinywa vya watoto walio na umri chini ya miaka 5

Wakizungumza na Mpanda Redio FM wananchi hao wamedai kuwa wengi wao wanatumia vitambaa na wengine kutumia mikono pasipo kujua njia sahihi za kitaalamu kwa ajili ya kusafisha vinywa vya watoto huku wakiiomba serikali kuwapa elimu.

Sauti za wananchi

Kwa upande wake mtaalam wa Afya ya kinywa na meno Kelvin Mlemi kutoka hospitali ya manispaa ya Mpanda ametaja njia sahihi za kusafisha kinywa cha mtoto. 

Sauti ya mtaalamu wa afya ya kinywa na meno

Aidha mlemi amesema kuwa mtoto asiposafishwa kinywa chake kwa njia sahihi inapelekea  harufu mbaya mdomoni  na kutoa wito kwa jamii kutowapa watoto vyakula vilivyo na sukari kwa wingi ili kuepuka kuharibika kwa fizi

Sauti ya mtaalamu wa afya ya kinywa na meno

 Afya ya kinywa kwa mtoto inaanza kipindi ambacho mtoto anaanza kuota jino moja na kuendelea hivyo mzazi anapaswa kuzingatia usafi wa kinywa cha mtoto.