Mpanda FM
Mpanda FM
19 February 2026, 2:22 pm

“Amepata majeraha baada ya kuchomwa kisu cha moto na mama yake mzazi kwa madai ya kuwa na tabia ya kuomba pesa kwa majirani“
Na Rhoda Elias-Katavi
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 4 ambae ni mkazi wa mtaa wa Mpanda Hotel kata ya Mpanda Hotel katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi amepata majeraha baada ya kuchomwa kisu cha moto na mama yake mzazi kwa madai ya kuwa na tabia ya kuomba pesa kwa majirani.
Wakizungumza na Mpanda redio FM jirani na ndugu wa karibu wa mtoto huyo wamedai kuwa mama wa mtoto amekua na tabia zisizofaa za kuadhibu watoto wake kupita kiasi
Nae Dachi Dadesi ambae ni mwenyekiti wa kikundi cha kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia mkoani Katavi (SUMAUJATA) ametaja sababu za ukatili huo kuwa ni changamoto za kifamilia .
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Ibrahim Msanda amekiri kuwepo kwa tukio hilo na tayari wamechukua hatua za kumpeleka mama huyo kituo cha polisi na kutoa rai kwa wakazi wa mtaa huo kuripoti matukio ya ukatili kwa ajili ya usalama wa watu wote.