Mpanda FM

Historia kuandikwa shule ya sekondari Mgombe

3 February 2026, 3:30 pm

Katikati ni mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akitembelea shule hiyo. Picha na Samwel Mbugi

“Mtunze kila kitu mnachokikuta kuanzia majengo mpaka samani”

Na Samwel Mbugi

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwananamvua Hoza Mrindoko amewataka wanafunzi na walimu wa shule ya Ufundi Mgombe secondary school iliyopo wilaya ya Mlele kijiji cha Uzega kutunza miundombinu ya shule hiyo.

Akizungumza mbele ya wanafunzi hao Mwanamvua amesema historia itakwenda kuandikwa kupitia wanafunzi ambao wamekuwa wa kwanza kuanza masoma katika shule hiyo.

Sauti ya mkuu wa mkoa

Joseph Emmanuel Lugongo ni makamu mkuu wa shule ya Mgombe secondary school amesema wanafundisha masomo ya kumuwezesha mwanafunzi kuwa na ujuzi  na maarifa kama vile ufundi magari na umeme.

Sauti ya makamu wa shule

Ikumbukwe kuwa kuanzishwa kwa shule za Ufundi ni maagizo ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ili vijana waweze kutumia fursa hiyo kujiajiri.