Mpanda FM
Mpanda FM
13 January 2026, 6:36 pm

Hayati Abeid Amani Karume. Picha na mtandao
“Hatuna uelewa wowote kuhusu Sikukuu ya Mapinduzi”
Na Anna Mhina
Wakati Zanzibar wakiadhimisha sikukuu ya Mapinduzi hapo jana January 12 baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kurithisha historia kwa vizazi vya sasa ili kuelewa umuhimu wa sikukuu hiyo.
Wakizungumza na Mpanda redio FM Baaadhi ya vijana wamesema kuwa hawana uelewa wa kutosha kuhusu maadhimisho haya ya sikukuu ya Mapinduzi hali iliyopelekea kuiomba serikali kutoa elimu ili kudumisha uzalendo wa historia ya nchi Ya Tanzania iliyoasisiwa na mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na hayati Abeid Amani Karume.
Thomas Msuba ni mzee wa mtaa wa Mpanda hotel ameeleza umuhimu wa maadhimisho hayo ikiwa Mapinduzi hayo yalikua chanzo cha kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania
Maadhimisho ya Mapinduzi hufanyika kila mwaka kama kumbukumbu ya tukio muhimu katika historia ya nchi na kama fursa ya kutafakari safari ya maendeleo yaliyofikiwa tangu wakati huo.