Mpanda FM
Mpanda FM
6 December 2025, 1:02 pm

“Mji wetu unapaswa uwe msafi”
Na Samwel Mbugi
Mkuu wa wilaya ya mpanda Jamila Yusuph amewataka madiwani wa kata zote za manispaa mkoani Katavi kusimamia usafi wa mazingira bila kusubiri wakuu wa idara husika ili kusaidia kutopata magonjwa yatokanayo na uchafu.
Ameyasema hayo wakati akizungumza katika barazara la madiwani ambapo amesema mji wa manispaa unapaswa kuwa msafi kila wakati wote kwa kushirikiana na wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji wa kata husika.

Kwa niaba ya madiwani wote wa manispaa ya Mpanda mstahiki meya Charles Philipo ambae pia ni diwani wa kata ya Magamba amesema suala la usafi wa mazingira wamelipokea na kwenda kulifanyia kazi ili kujinusuru na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Charles amesema watashirikiana vizuri na wakuu wa idara ili kuhakikisha manispaa ya Mpanda inakuwa ni mfano wa kuigwa kwenye suala la usafi wa mazingira.