Mpanda FM

6 Desemba kubadili mitazamo ya wanawake Katavi

17 November 2025, 12:31 pm

Mwanzilishi wa Katavi worth women Leah Gawaza. Picha na Anna Millanzi

“Matukio haya yote yanalenga kumsukuma mwanamke kuleta mafanikio”

Na Anna Millanzi

Uongozi wa Katavi Worth Women umezindua msimu mpya wa kutoa hamasa kwa wanawake na kuwakutanisha pamoja ili kuendelea kupeana maarifa ya kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na Waandishi wa habari na baadhi ya wanawake waliohudhuria mkutano huo mwanzilishi wa Katavi worth women Leah Gawaza amesema wameanza kufanya matukio hayo tangu mwaka 2022 lengo hasa ikiwa ni kuleta mafanikio ya kijamii.

Sauti ya Leah Gawaza

Sambamba  na Hayo Leah ameeleza kuwa tukio hilo litafanyika Likiwa na mada mbalimbali na utolewaji wa tuzo kwa wanawake waliopendekezwa kuwania tuzo hizo kwa vipengele mbalimbali.

Sauti ya Leah Gawaza

Wanawake walioshiriki mkutano huo  wamesema uwepo wa katavi worth women umewasaidia sana kujiinua kiuchumi.

Sauti ya washiriki

December 6,2025 wanawake mkoani katavi wataungana pamoja kusherehekea ,kubadilishana mawazo na kupeana fursa huku tukio hilo wakilipa kaulimbiu isamayo katavi worth women jitathimini