Mpanda FM
Mpanda FM
22 October 2025, 1:57 pm

Waumini wa kanisa la Living Water wakihitimisha maombi. Picha na Anna Mhina
“Nazidi kuwasisitiza viongozi Taifa bado linahitaji kumuomba Mungu”
Na Anna Mhina
Waumini wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Living Water lililopo mtaa wa Kwalakwacha kata ya Nsemulwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamefanya maombi ya siku kumi na nne (14) kwa ajili ya kuombea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 29 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kilele cha maombi hayo katibu wa idara ya maombi Lucas Nyangasa ameeleza lengo la kufanya maombi hayo ni kuombea uchaguzi kwani wanaamini katika maombi kila kitu kinawezekana huku mhadhini wa idara hiyo Elizabeth Samwel amewashukuru waumini kwa kujitokeza katika maombi hayo.
Kwa upande wao baadhi ya waumini waliohudhuria kwenye maombi hayo akiwemo Fortune Manjem, Sifa Pascal na Greyson Nichorus wameeleza namna walivyopokea kwa furaha tangazo la kuombea uchaguzi na kuamini kuwa watapokea majibu mazuri.
Maombi hayo ya siku 14 yaliyolenga kuombea uchaguzi wa haki na amani yalianza rasmi October 6, 2025 na kutamatika October 19, 2025.