Mpanda FM

Mbukwa: Wamehitimu elimu ya msingi hawajamaliza shule

18 September 2025, 10:33 am

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Katavi Judith Mbukwa. Picha na Anna Mhina

“Hawa watoto ni wanafunzi ambao wapo likizo kusubiri matokeo yao”

Na Anna Mhina

Wazazi na walezi wametakiwa kuacha tabia ya kuwatumia watoto kama mtaji pindi wanapohitimu elimu yao ya msingi na badala yake wawaache wafikie ndoto zao.

Hayo yamesemwa na   mkaguzi wa polisi Judith Mbukwa ambaye pia ni mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Katavi kutokana na kuwepo kwa tabia ya baadhi ya wazazi kupokea posa na kuwatafutia ajira watoto wao pindi wanapohitimu darasa la saba.

Sauti ya mkuu wa dawati la jinsia

Kwa upande wao baadhi ya wazazi na walezi wa kata ya Mpanda hotel wameeleza sababu za kuwapa majukumu yakujitafutia kipato watoto hao ikiwemo hali ngumu ya maisha ya wazazi huku wengine wakieleza namna wanavyowalinda watoto wao kwa kuwaendeleza na masomo ya kabla ya kidato cha kwanza yaani pre form one.

Sauti ya wazazi