Mpanda FM
Mpanda FM
16 September 2025, 3:31 pm

“Mgombea udiwani Kata ya Nsemulwa na kata ya Shanwe wamemuombea kura mgombea udiwani wa kata hiyo ya kazima“
Na Anna Milanzi-Katavi
Chama cha ACT wazalendo kimeendelea na kampeni zake katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi na kunadi sera zao kwa wananchi.
Wakizungumza katika viwanja vya kazima manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wagombea udiwani akiwemo mgombea udiwani kata ya kazima amewaomba wananchi wamchague yeye ili alete maendeleo katika kata hiyo huku mgombea udiwani Kata ya Nsemulwa na kata ya Shanwe wamemuombea kura mgombea udiwani wa kata hiyo ya kazima pamoja na mgombea ubunge wa Mpanda mjini kupitia chama hicho cha ACT Wazalendo.
Mgombea ubunge jimbo la Mpanda mjini kupitia chama hicho cha ACT wazalendo amesema kuwa endapo wakimchagua atahakikisha anaweka kipaumbele upatikanaji wa maji ya uhakika,elimu,upatikanaji wa umeme wa uhakika,kuondoa kero zinazowakumba wasafirishaji,uboreshaji barabara na kuyasaidia makundi maalumu.
Vyama mbalimbali mkoani Katavi vinaendelea na kampeni na kunadi sera zao kwa wananchi,ikumbukwe kuwa kampeni hizi zitafika ukomo tarehe 28 mwezi October 2025 na uchaguzi mkuu utafanyika October 29,2025.