Mpanda FM

Wananchi Mpanda waomba elimu ya mikopo

10 September 2025, 1:06 pm

Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Mpanda Irene Samson. Picha na Leah Kamala

” Tunapata pesa lakini hatujui namna ya kuitumia hivyo ni muhimu kupata elimu”

Na Leah Kamala

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kutoa elimu ya mikopo ili wajue namna bora ya kukopa na kutumia mikopo kwa shughuli za kimaendeleo.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wameongeza kuwa kupitia elimu hiyo ya mikopo itawawezesha kurejesha mikopo kwa wakati.

Sauti za wananchi

Nae afisa mandeleo ya jamii manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Irene Samson amesema kuwa elimu ya mikopo ni muhimu kutolewa ili kuwafanya wananchi wawe na mazoea ya kupanga matumizi bora ya kutumia mikopo hiyo.

Sauti ya afisa maendeleo ya jamii

Elimu ya mikopo ni nyenzo muhimu kwa wananchi, iwapo wananchi watapewa elimu ya kutosha watakopa kwa uangalifu na kutumia mikopo hiyo ipasavyo na kusaidia kuchangia maendeleo yao na taifa kwa ujumla.