Mpanda FM
Mpanda FM
4 September 2025, 4:12 pm

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Sifa Mwanjala. Picha na Samwel Mbugi
“Semina hii inalenga namna ya kupambana na rushwa katika uchaguzi mkuu”
Na Samwel Mbugi
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Katavi imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari, watendaji wa kata na walimu walezi wa klabu za kupinga vitendo vya rushwa kwa shule za msingi na Sekondari.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Sifa Mwanjala amesema lengo la mafunzo hayo ni kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 Mwaka huu.
Pia Mwanjala amewaasa waandishi wa habari kutumia vyema taaluma yao na kufikisha elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wananchi ili kudhibiti vitendo hivyo.
Hata hivyo washiriki wa mafunzo hayo wametoa maoni yao kwa TAKUKURU namna ambavyo wanaweza kufanya ili kupunguza vitendo vya rushwa hususani katika kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi mkuu ikiwa ni pamoja na kuwa karibu na jamii.
Hata hivyo mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Sifa Mwanjala amesema ni vyema wananchi kutoa taarifa juu ya uwepo wa vitendo hivyo kwenye jamii ili kupata viongozi wasiotokana na vitendo vya rushwa ambapo kauli mbiu inasema “KUZIA RUSHWA NI JUKUMU LAKO NA LANGU,TUTIMIZE WAJIBU WETU”.