Mpanda FM
Mpanda FM
4 September 2025, 10:38 am

” Kukaa na mkojo kwa muda mrefu kunaweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi”
Na Anna Mhina
Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuacha tabia ya kubana haja ndogo kwa muda mrefu (mkojo) ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza.
Akizungumza na Mpanda Radio FM, mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Town Clinic Gabriel Elias ameeleza madhara yatokanayo na kukaa na mkojo kwa muda mrefu ikiwemo U.T.I sugu pamoja na kusababisha figo kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Baadhi ya wananchi wa Mpanda Hotel wameeleza sababu zinazosababisha kukaa na haja ndogo muda mrefu kuwa ni uvivu, matumizi ya simu, kujali biashara, ukosefu wa elimu juu ya madhara ya kitendo hicho na hofu ya matumizi ya vyoo visivyo salama hasa maeneo ya biashara.
Kukaa na haja ndogo kwa muda mrefu kunachangia uwezekano wa kuunda mawe kwenye kibofu cha mkojo kutokana na mkusanyiko wa chumvichumvi zilizopo na kusababisha maumivu makali na kuziba kwa mirija hiyo .