Mpanda FM
Mpanda FM
17 August 2025, 3:15 pm

“kikao cha halmashauiri kuu kupitia chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi kilichofanyika August 13,2025 kimewateua wagombea udiwani katika kata hizo“
Na Anna Milanzi-Katavi
Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi kimeteua majina ya wagombea udiwani katika kata 58 zilizopo mkoani humo.
Akitangaza majina ya wagombea udiwani walioteuliwa August 17,2025 katika ofisi za chama cha mapinduzi mkoa wa Katavi ,Katibu wa siasa na uenezi CCM Teonas Kinyonto amesema kikao cha halmashauiri kuu kupitia chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi kilichofanyika August 13,2025 kimewateua wagombea udiwani katika kata hizo ili kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika October 29,2025
Katika wilaya ya Mpanda jimbo la Nsimbo pamoja na manispaa ya mpanda jimbo la Mpanda amewataja pia walioteuliwa kuwania udiwani katika kata za majimbo hayo huku baadhi ya majina yakiwa ni majina ya waliowahi kuwa madiwani katika kata hizo.
Kupitia majina hayo yaliyosomwa yanaonyesha idadi ndogo ya wanawake watakaogombea udiwani kupitia chama hicho ambapo Kinyonto amesema walipita kila mahali kuhamasisha wanachama wa chama hicho kujitokeza kushiriki katika mchakato huo wa uchaguzi.
Kinyoto amewapongeza wanawake wote waliojitokeza katika mchakato wa kuchukua fomu na kugombea lakini pia amewapongeza walioteuliwa kugombea udiwani katika kata zao.