Mpanda FM
Mpanda FM
13 August 2025, 4:58 pm

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamil Yusuph. Picha na Samwel Mbugi
“Tumedhamiria kufanya maonesho kabla yamsimu wa kilimo”
Na Samwel Mbugi
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewapongeza wakulima na wajasiriamali walioenda kwenye maonyesho ya Nanenane jijini Mbeya kwa kuiwezesha halmashauri ya Mpanda kushika nafasi ya tatu katika maonyesho.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema maonyesho ya nanenane yametumika kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo pamoja na ufugaji ulio bora.
Pia jamila amesema kuwa wilaya ya Mpanda imejiweke mikakati na mipanga katika kuhakikisha ujuzi walioupata kupitia maonyesho hayo unawafikia wananchi wote kwa kuandaa eneo litakalotumika kutoa elimu hiyo kabla ya msimu wa kilimo.
Ikumbukwe kuwa maonyesho ya nanena mwaka huu kitaifa yamefanyika jijini Dodoma na kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.