Mpanda FM

Wakulima watumieni vema maafisa kilimo

12 August 2025, 11:58 am

Ndugu Adili Mbilinyi akitoa neno kwa wakulima. Picha na Leah Kamala

“Nitoe wito kwa wananchi watumieni vema maafisa kilimo”

Na Leah Kamala

Baadhi ya wakulima wa Kitongoji cha kasherami A, Kijiji cha muungano kata ya Ibindi halmashauri ya Nsimbo wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia kanuni bora za kilimo.

Mafunzo hayo yamefanyika katika uwanja wa muungano huku afisa kilimo halmashauri ya Tanganyika Neema Mbuya amewaeleza wakulima wa kijiji cha Ibindi kanuni za kilimo bora ili waweze kuzalisha kwa tija na kupata mazao mengi.

Sauti ya Neema Mbuya

Aidha akizungumzia dira ya kilimo ya Taifa afisa kilimo halmashauri ya nsimbo Leah Mhando amesema kuwa dhamira ya dira hiyo ni kutengeza sekta ya kilimo endelevu inayolenga katika kukuza uchumi jumuishi.

Sauti ya

Akimwakilisha mgeni rasmi katika hafla hiyo ndugu Adili Mbilinyi amewasisitiza wakulima wa Kijiji cha Ibindi kuwatumia vyema wataalamu wa kilimo ili kuweza kufanikisha kilimo chenye mafanikio.

Sauti ya mgeni rasmi

Kilimo bora ni chachu ya maendeleo ya wakulima na uchumi wa taifa kwa ujumla kupitia elimu na mbinu za kisasa wakulima wanapata fursa ya kuongeza mavuno, kuboresha kipato na kuhakikisha usalama wa chakula katika jamii.