Mpanda FM
Mpanda FM
7 August 2025, 4:56 pm

Muuguzi katika hospitali ya manispaa ya MpandaAnderson Evarist Fidel. Picha na Samwel Mbugi
“Tunachowasaidia tunamchukua mtoto na kumuweka kwenye maziwa ya mama”
Na Anna Millanzi
Kina mama wanaojifungua watoto manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia unyonyeshaji wa watoto wao .
Akizungumza na Mpanda Redio FM Shalon Nerson Muuguzi mfawidhi wa hospitali ya manispaa ya Mpanda ameeleza faida kwa mama aliyejifungua kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja mara baada ya kujifungua.
Afisa lishe manispaa ya Mpanda Mwanaidi Salimu amesema ni muhimu kwa mama aliyejifungua kumnyonyesha mtoto bila kumpa kitu chochote kwa kipindi cha miezi sita na baada ya kuanza kumpatia chakula mtoto anapaswa kunyonyeshwa si chini ya miaka miwili.
Afisa muuguzi katika hospitali ya manispaa ya Mpanda Anderson Evarist Fidel ameeleza changamoto wanazokutana nazo ikiwemo mama aliyejifungua kutotoa maziwa kwa wakati.
Mariam shabani ni mama wa watoto watano anatueleza namna ambavyo anazingatia kunyonyesha watoto wake na kueleza faida anayoiyona katika malezi hasa kunyonyesha watoto kwa kuzingatia taratibu za afya.
Wiki ya Unyonyeshaji Duniani imeanza august mosi na inatamatika august 7 mwaka huu ambapo Takwimu zinaonesha nchini TANZANIA watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya Mama mpaka umri wa miaka miwili au Zaidi ni asilimia 62 na mwaka huu kauli mbiu inasema“Thamini Unyonyeshaji, Weka Mazingira wezeshi kwa Mama na Mtoto”.